Header Ads

Breaking News
recent

Msanii Ruby afunguka kuhusu Nandy.

Mwanamuziki Ruby aliyefanya poa na ngoma ya 'Na Yule' amewataka mashabiki zake wasijichanganye kwa kumfananisha na Mwanamuziki 'Nandy' anayetamba  sasa na ngoma  'Wasikudanganye' kwa kuwa kamwe msanii huyo hawezi kufanya vitu ambavyo yeye anafanya. 

"Nandy ni msanii wa kike ambaye ni chipukizi  amenikuta kwenye game mimi ni msanii mkubwa sana kwake, kwa Vitu anavyovifanya mimi ninauwezo wa kufanya zaidi yake. Watu wakisema kwamba ameniacha mbali kimuziki watakuwa wanakosea kwani mimi ni wa kwanza kuliona jua kabla yake," Ruby amefunguka


Pamoja na kufananishwa aina ya uimbaji wao Ruby ameongeza kwamba " Nandy nimeshawahi kukutana naye mara chache na niseme hawezi kuimba kama mimi. Ila mimi Ruby nina uwezo wa kuimba kama yeye na labda siku moja ninaweza kuimba kama anavyofanya Nandy  ili watu wasitufananishe tena".

"Siwezi kutoa nyimbo mfululizo lakini nitoe ahadi sitaweza kukaa kimya tena .
Chanzo: Eatv

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.