Header Ads

Breaking News
recent

Aamir Khnan ahamasisha watu kujitolea kuwasaidia watu walioathiriwa na mafuriko Gujarat India

Hali  ya maeneo ya Gujarat nchini India sio nzuri, ikiwa ni baada ya hivi karibuni kukumbwa na mafuriko makubwa, yaliyosababisha kupoteza maisha ya takribani watu 120 na hasara mbali mbali.
Pamoja na mafuriko ya hivi karibuni yaliyotokea, serikali imekuwa na hasara kubwa. Superstar Aamir Khan amechukua time kupitia ukurasa wake wa Twitter kuonesha huzuni yake juu ya kupoteza maisha na makazi ya watu.

Katika video aliyoiweka Twitter Aamir ameonekana akiwahamasisha watu kuchukua hatua ya kuwasaidia wakazi wa Gujarat ambao takribani 10,000 kutoka maeneo ya vijijini na mijini wamekosa sehemu ya kuishi.
Aamir anajulikana kwa huduma zake za kijamii na kuwakumbusha watu wajibu wao, kwa wananchi wenzake. 

Katika siku za nyuma pia, amewahi kujitoa kuhamasisha watu kujitoa katika kuisaidia jamii.
Hii pia ni hatua muhimu sana iliyochukuliwa na Aamir ili kuwasaidia watu wa Gujarat.

 Star huyu hivi karibuni ataonekana katika movie mpya ya Secret of Superstar, iliyopangwa kuachiwa mwezi Oktoba

Mbali na hilo, sasa anafanya kazi kwenye katika filamu ya Thug of Hindostan na star Amitabh Bachchan, Fatima Sana Shaikh na Katrina Kaif.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.