Header Ads

Breaking News
recent

Top 10 ya mastaa wakike wenye macho mazuri zaidi duniani.

Macho ni kiungo ghari na muhimu katika uso wa mwanadamu. Sasa leo wakwetu nimekutana na hii ya mastaa wakike duniani wenye macho mazuri zaidi, huenda wewe ukawa unawako unaye mfahamu, lakini hawa ni wale 10 maarufu waliotajwa.

Wanasema macho ya mwanamke ni asset nzuri zaidi katika mwili wake. Kwani anaweza kuonyesha hisia zake na furaha yake kupitia macho, anaweza kuongea kwa kwa kutumia macho na ukamuelewa. Ni ngumu sana kukutana na macho mazuri, lakini sasa cheki hawa wakali hapa>>> 

10. CHARLIZE THERON
Charlize Theron ni muigizaji na mwanamitindo kutoka Afrika ya Kusini. Alianzia kazi ya uigizaji Marekani na kuwa maarufu miaka ya 1990 hivi . Ana macho mazuri. Pia amekwisha kushinda tuzo ya Oscar kama Best Performance kama staa wa kike katika filamu ya Monster.

9. MILLA JOVOVICH
Milla Jovovich ni mwanamitindo, muigizaji, mwanamuziki na mbunifu wa mavazi. Katika kazi zake amekwishaonekana katika filamu za kiasayansi na zile za action huku katika muziki akipewa umaarufu kama “reigning queen of kick-butt”.

8.CELINA JAITLEY
Celina Jaitly ni muigizaji wa kike kutoka India ambaye amekua akionekana katita filamu za Bollywood. Pia Celina alikuwa ni beauty queen na model pia, amekwisha shinda mashindano ya umiss na kutwaa taji la Femina Miss India Universe mwaka2001.

 7. KRISTIN KREUK
Kristin Laura Kreuk ni muigizaji na muandaaji mkuu wa filamu kutoka Canadia. Ukitaka kumfahamu vizuri zaidi, cheki series ya kimarekani inayoitwa Smallville, ameigiza kama Lana Lang

6. GIADA DE LAURENTIIS
Giada Pamela De Laurentiis ni mpishi, mwandishi, na mtangazaji wa Tv Imuitalia na mmarekani. Anakipindi chake cha kinachohusu mapishi ambacho huruka kila siku katika Food Network tangu 2003.

5. AUDREY HEPBURN
Audrey Hepburn alikuwa ni muigizaji na liyejihusisha na masuala ya kijamii kutoka Uingereza. Audrey alishawahi kushinda tuzo ya  Oscar kama muigizaji bora wa kike.

4. ELIZABETH TYLOR
Dame Elizabeth Rosemond “Liz” Taylor, DBE alikuwa ni muigizaji wa kike mwenye asili ya British-American. Ameshawahi kushinda tuzo mbili za Oscars, moja wapo ikiwa ni kuhusu macho yake mazuri. 

3.KRISTIN STEWART
Kristen Jaymes Stewart ni muigizaji wa kike kutoka Marekani, maarufu kama staa aliyecheza Bella Swan katika movie ya The Twilight Saga. Kristen Stewart ana macho yenye mvuto ambayo kila mtu atanasa akimtazama.

2. ANGELINA JOLIE
Angelina Jolie ni muigizaji na muongozaji wa filamu kutoka Marekani. Angelina amekwisha shinda tuzo ya Academy, mbili za Screen Actors Guild Awards, na tatu za Golden Globe Awards, yeah macho yake yanamvuto na midomo yake yakuvutia. Angelina ni binti ya Jon Voight na amekwisha wahi kushinda tuzo ya Oscar kama muigizaji msaidizi bora wa kike.

1. AISHWARYA RAI
Aishwarya Rai ni muigizaji maarufu wa filamu kutoka India. Mwanzoni alifanya kazi kama mlimbwende/model, na hatimae akashinda Miss World pageant mwaka 1994

Hakika macho yake yanadhirika kuwa yenye mvuto dunia nzima na kumfanya kushika nafasi ya kwanza katika mastaa wa kike wenye macho mazuri zaidi duniani.

Aishwarya alikwisha kuchaguliwa na Time magazine mwaka 2004 kama mmoja kati wa "watu 100 wenye ushawishi duniani" na anatambulika pia kama mwanamke mrembo zaidi duniani.

Je unamaoni gani kuhusu hii orodha iliyoandaliwa na mtandao wa wonders list?

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.