Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SASA FURAHIA KUTIZAMA (ASILI TV ONLINE) KILA WAKATI

June 19, 2017

Beyonce na Jayz wapata watoto mapacha.

Mastaa wa muziki duniani kutoka Marekani yani Beyonce Knowles na Sean Carter 'Jay Z' inavyosemekana wamewakaribisha mapacha wawili, baada ya Bey kutumia muda wake wa ujauzito kikamilifu na kuweza kujifungua salama, huku watoto wakiwa na afya njema kwa mujibu wa mtandao wa 'TME'.

Kwa vyanzo mbali mbali vya kimataifa, vimeeleza kuwa waili hao bado hawajasema chochote, kuhusu Bey kujifungua, ila inasemekana mambo tayari, na muda ukifika watatuwekea watoto hadharani tuone wamechukua sura kwa nani, baba au mama. 

Blue Ivy Carter ni mtoto (binti) yao wa kwanza, toka wanandoa hao wenye nguvu zaidi duniani kufunga ndoa mnamo mwaka 2008, na kumkaribisha binti yao wa kwanza aitwae Blue mwezi  January 7, 2012.