Header Ads

Breaking News
recent

Baba yake Beyonce, Mathew athibitisha kuzaliwa kwa watoto mapacha wa mastaa Jayz na Beyonce.

Baada ya kusambaa kwa tetesi za Beyonce na Jay Z kupata mapacha.
 Baba mzazi wa Queen Bey ambaye pia aliwahi kuwa meneja wake, Mathew Knowles amethibitisha hilo.

 Jumapili hii  Knowles aliweka picha ya kadi kwenye mtandao wa Twitter akipongeza kuzaliwa kwa mapacha hao na kuandika, “They’re here! #beyonce #twins #jayz #happybirthday.”

Katika kuthibitisha jambo hilo ni kweli, baba huyo wa msanii Beyonce aliweka picha hiyo hiyo kwenye mtandao wa Instagram na mama yake Beyonce aliweza ku-like picha hiyo.

Kwa mujibu wa TMZ, inadai kuwa watoto hao wamezaliwa Jumatatu iliyopita ya Juni 12 lakini mpaka sasa bado wapo hospitalini hawajaruhusiwa wakiwa chini ya uangalizi pamoja na mama yao.
Blue Ivy Carter ni mtoto (binti) yao wa kwanza, toka wanandoa hao wenye nguvu zaidi duniani kufunga ndoa mnamo mwaka 2008, na kumkaribisha binti yao wa kwanza aitwae Blue mwezi  January 7, 2012.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.