Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

TAZAMA KIONJO CHA JIBAMBEE TV SHOW

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

May 9, 2017

Pale Rubanii anapolala kwenye ndege.

Rubani wa shirika la ndege la Pakistan ,Amir Akhtar Hashmi, amesimamishwa kazi baada ya kuonekana kwenye picha zilizopigwa na abiria pindi walipomuona amelala.

Rubani huyo alilala na kumuachia ndege rubani wa ziada ambaye bado yuko kwenye mafunzo. Ndege hiyo ilikua inaruka kutoka Pakistan kwenda London.

Msemaji wa shirika la ndege la Pakistan International Airline (PIA), amesema kuwa rubani huyo aliyelala alikuwa akihatarisha maisha ya abiria 305 waliokuwepo kwenye ndege hiyo.

Kaptain Amir Akhtar Hashmi alitumia masaa mawili na nusu kulala sehemu ya abiria ya business class, mnamo tarehe 26 aprili. 

Ndipo abiria walipoona na kupiga picha hiyo na kabla ya kufika Uingereza abiria waliamua kuripot tukio hilo.