Header Ads

Breaking News
recent

Nimeacha Foundation inawakaribisha wadau kuungana kwa pamoja katika kuwatembelea watoto wenye ulemavu Arusha.

Nimeacha Foundation Limited ni shirika lisilokuwa la kiserikali yani 'non profit Organisation' lilopo mjini Arusha, sasa linayofuraha kuwakaribisheni kuungana na "Nimeacha Youth Club" (umoja wa vijana wa Nimeacha) katika kutembelea kituo cha watoto wenye ulemavu wa viungo na usonji alhamisi hii ya May 4th , 2017 katika shule ya msingi Leganga Arusha.

Watoto hawa wanahitaji msaada wako, japo hata kukaa nao kwa muda mfupi tu, itakua ni faraja kubwa kwao.

Kama unapenda kuwa sehemu ya tukio hili, tafadhali wasiliana nasi kupitia>>>>> 0765 282 876, nimeacha2016@gmail.com, www.facebook.com/NimeachaFoundation
 
Na kama utaguswa kutoa msaada wa nguo, dawa ya meno, miswaki, sabuni, number boards au kitu chochote kile tujulishe, nasi tutakuja kuvichukua!
Asante!

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.