Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

March 20, 2017

Yanga yatupwa nje ligi ya mabingwa Afrika, sasa kucheza kombe la Shirikisho

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga imeangukia tena kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na Zanaco FC kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa uliopo mjini Lusaka Zambia.

Matokeo hayo yanamaanisha Yanga inatolewa kwa bao la ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 


 ZANACO FC wao wametinga hatua ya makundi na Yanga itawalazimu kusubiri droo ya kombe la Shirikisho ili kujua watakutana na timu gani.

Timu nyingine ya Tanzania, Azam FC imetupwa nje ya michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kufungwa na wenyeji Mbabane Swallows goli 3-0 nchini Swaziland.