Header Ads

Breaking News
recent

Kalamu za kipelelezi na zenye uwezo wa kurekodi sauti na video HD.

Kila kukicha wanasayansi wanagundua vitu vya mbele zaidi ili kuweza kutatua na kurahisisha maisha na kazi za walimwengu. Sasa kwa hali ya kawaida wakwetu unafahamu matumizi ya kalamu ni kuandika tu na si vingine.
Sasa nimekutana hii stori ya kalamu za kispy/kipaparazi ambazo zinauwezo tofauti na kawaida. 

Mbali na kutumika kuandika pia kalamu hizi zimewekewa DVR (Digital Video Recorder) yenye uwezo wa kamera HD inayoweza kutumika kunasa picha na video zenye ubora wa hali ya juu.
Kalamu hizi zinaweza kutumika kawaida kuandikia na pia zinaweza kutumika kama flash, huku zikiwa zimetengenezewa betrii za kuweza kuchajiwa na kukaa na umeme. Kumbuka video zake zinaweza kuwekwa kwenye komputa na kutazamwa.

Kwa stori za teknolojia endelea kutembelea blog hii na karibu ulike ukurasa wetu wa Facebook - ASILI YETU TANZANIA

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.