Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

February 1, 2017

Viongozi wapya wa Umoja wa Afrika waapishwa.

Viongozi wapya wa ngazi ya juu wa Kamati ya Umoja wa Afrika, akiwemo mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo wameapishwa jana wakati wa kumalizika kwa mkutano wa kikao cha 28 cha umoja huo uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Maofisa wengine walioapishwa ni pamoja na wale wa amani na usalama, masuala ya kisiasa, biashara na viwanda, masuala ya kijamii, miundombinu na nishati, na uchumi wa vijijini na kilimo.
Katika mkutano huo, rais Alpha Conde wa Guinea alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika.


Wakati huohuo, Umoja wa Afrika umeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na washirika wengine kuunga mkono zaidi kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Source: CRI