Header Ads

Breaking News
recent

Rihanna avunja rekodi ya Michael Jackson kwa nyimbo.

Rihanna amempiku Michael Jackson katika kuwa na nyimbo katika chati ya nyimbo kumi bora nchini Marekani.

Hii ni baada ya wimbo wake mpya wa Love on the Brain kuingia kwenye orodha hiyo.

Huo unakuwa ni wimbo wake wa 30 kuwa kwenye chati hiyo, na sasa ameachwa nyuma na The Beatles na Madonna pekee.

Madonna ana nyimbo 38 zilizowahi kuwa kwenye chati hiyo. The Beatles wana nyimbo 34.
Michael Jackson, au mfalme wa pop duniani aliyefariki Juni 2009, alikuwa na nyimbo 29 katika chati hiyo ya nyimbo kumi bora.

Mwaka 2005, wimbo wa Rihanna wa Pon De Replay ulikuwa namba mbili katika chati za muziki nchini Marekani na Uingereza.

ImemchukuaRihanna miaka 10, miezi saba na wiki mbili kuwa na nyimbo 30 kwenye chati ya nyimbo bora nchini Marekani.

Sii kazi rahisi kuingia katika orodha hii, nyimbo za Madonna zilizovuma aliziachia katika kipindi cha miaka 13.

The Beatles walifika hapo kwa kutumia miaka mitano, miezi tisa na wiki mbili pekee.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.