Header Ads

Breaking News
recent

Radio na Weasel wajishindia nafasi ya kufanya Remix na Soop Dogg.

Wasanii wa kundi la Good Lyfe kutoka Uganda wamepata mchongo wa kufanyia remix ngoma yao ya "Plenty Plenty" ambayo ndio wanayotamba nayo hivi sasa. Wimbo huo wataufanya na msanii wa hip hop kutoka Marekani unaweza kumuita Snoop Dogg. Wasanii hao kwa sasa wako katika harakati za kushuti video na msanii Snoop Dogg.

Wakali hao mwanzoni walishuti video ya "Plenty plenty" Johannesburg, Afrika ya Kusini mwaka jana 2016 na sasa wako katika harakati za kushuti na msanii Snoop katika maeneo ya Hollywood nchini Marekani.

Wakizungumza na BET Africa, wasanii hao kutoka Uganda wameelezea furaha yao kuhusu hiyo collable kuwa, Snoop ni msanii ambaye wamekua wakiwa wanamsikiliza na ndiye aliyewavutia kuupenda muziki.


Kama bado hujatupia macho wimbo wao wa "Plenty Plenty" basi utizame hapo chini.... 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.