Header Ads

Breaking News
recent

Mambo matano ya kuvutia kuhusu Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Bara la Afrika ni bara lenye utajiri mwingi sana duniani, lakini pia ni bara la kitofauti sana kutoka na utalii uliyomo kwamfano, milima, mabonde, maporomoko, wanyama, utamaduni n.k

Sasa leo wakwetu nakusogezea hivi vitu vitano tu katika upande wa wanyama vinavyo weka headline wakati wote...
  • Mnyama mkubwa kabisa duniani anayeishi nchi kavu (tembo) hupatikana Afrika.
  • Mnyama mrefu kuliko wote duniani, ni twiga, anaishi Afrika.
  • Mnyama mwenye kasi kubwa kuliko wanyama wote ni duma, anaishi Afrika.
  • Mamba wakubwa kabisa duniani ni mamba wanaoishi mto Nile uliopo Afrika.
  • Nyani mkubwa kabisa duniani anapatikana katika misitu ya Afrika.
Afrika bado itabaki kuwa ni sehemu ya utalii siku zote, endapo utalinda na kuhifathi maliasili zilizopo, kama vile misitu, wanyama na ardhi pia.

Tanzania inavivutio vingi sana vya kuweza kukustarehesha na ukasahau nchi nyingine, karibu utembelee mbuga zetu za wanyama, tusiwaachie tu wageni kutoka mataifa mbalimbali, twende Serengeti, Manyara, Kilimanjaro, Ngorongoro, Katavi, Mikumi na mbuga nyinginezo, tukaone nyumbu wengi kama nyasi, simba, tembo, faru n.k.

Fuatilia makala nyingine inayohusu utalii wa Tanzania na Afrika kwa ujumla....

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.