Header Ads

Breaking News
recent

Mambo 5 unayopaswa kukabiliana nayo katika siku ya Valentine's Day na siku za kawaida.

Siku ya Valentine wengi huitumia kusherehekea mahusiano yao na kuweka mambo yao sawa, ikiwa ni pamoja na kununuliana zawadi, kutoka out kidogo na rafiki, familia na wengineo.

Lakini pamoja na hayo hakuna kitu kisichokuwa na hasara labda tu kumwabudu Mwenyezi Mungu  ndio hakuna hasara na ni baraka tele.

Sasa siku hii kwa wengine hugeuka kuwa chungu kweli, ikiwa ni pale unapofahamu kuwa mwenzi wako ana kazi za nje (michepuko) au anatumia siku hiyo kukuambia 'it's over'.

Hivi ni vitu vitano muhimu unavyopaswa kuzingatia katika siku kama hizi za kuazimisha upendo na hata siku za kawaida unapokutana na rafiki yako.

5. Unapokuwa na marafiki zako au mwenzi wako na hamjaingia katika ndoa, usikubali kunywa vitu ambavyo hujawahi kuvitumia, kwa mfano pombe. Na hata kama unakunywa kunywa kiasi kisicho sababisha kubadili mtizamo wako wa mwanzo, huenda mwenzio akatumia kigezo cha pombe kukulewesha then akala tunda hata bila kutumia kinga.

4. Tumia kinga unapofanya mapenzi, kwani huezi jua maambukizi yapo kila siku na njia hizo zipo chungu mzima.

3. Ni vizuri mkasherehekea sehemu za wazi bila kificho, hii inasaidia kupima uaminifu wenu, na endapo mwenzi wako anakuficha ficha mara chumbani guest, basi hilo pia ni swali la kujiuliza huenda akawa na msululu.

2. Usikubali mwenzi wako kuzima simu yake, ikibidi mwambie aweke kabisa mlio, kama ilikuwa ni silence au Vibration. Hii inamaana yake hii itakusaidia kujua kama anamahusiano na mtu mwingine zaidi yako.

1. Jiandae kwa lolote kutoka kwa yule umpendae, kama leo atasema tuishie hapa, basi  ujue kwamba huyo mtu hukuzaliwa nae, mlikutana nae tu ukamthamini na kumuingiza katika ndoto zako.

Usiumie sana moyo, huenda kuondoka kwako katika maisha yako kakuepusha vitu vingi, so make another choice, ila usikurupuke kutoka na mtu mwingine ili kumkomoa wa zamani hapo utakuwa unaharibu zaidi.

Tulia kwanza chunguza na ubaini mtu mwingine mwenye sifa unazozihitaji, sio lazima afanane na yule wa mwanzo kitabia, hapana kila mtu anauzuri wake.

Asante sana kwa kusoma makala hii, zipo nyingine nyingi tu zinakujia, endelea kufuatilia Asili Yetu Tanzania Blog.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.