Header Ads

Breaking News
recent

Maajabu: Watalii wawili kwenda kufanya utalii mwezini.

Mwezini ni sehemu ya anga ambayo ni mbali sana na dunia tunayoishi na imewachukua muda mrefu sana wanasayansi kuweza kufika huko. Eneo la mwezini kwasababu ya umbali wake na hali ya hewa, imepafanya kuwa sehemu ya utafiti tu kwa miaka mingi.

Lakini leo nimekutana na hii stori ya kuwapeleka watalii wawili waliolipa pesa kwenda mwezini, unadhani watakuwa wamelipa kiasi gani? anyway bilashaka na wewe huenda ikawa imekushangaza, endelea hapo chini....

Kampuni ya kibinafsi ya kurusha roketi imetangaza kwamba watalii wawili wamelipa kupelekwa mwezini.
Safari hiyo itafanyika 2018 kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.

“Hatua hiyo inatoa fursa kwa binaadamu kurudi katika anga za juu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45″alisema.

Wawili hao ambao majina yao hayakutajwa wataelekea mwezini wakiwa katika meli hiyo ya angani ambayo itafanyiwa jaribio lake la kwanza la kurusha rekoti isiokuwa na rubani.

Bwana Musk alisema kuwa ushirikiano wa shirika la sayansi na teknolojia ya angani nchini Marekani Nasa umefanya ufanisi wa safari hiyo.

Amesema kuwa abiria hao wawili watasafirishwa kwa kasi zaidi ya watu wengine wowote kuwahi kusafirishwa katika sayari.

Bwana Musk hatahivyo amekataa kuwataja abiria hao wawili ,akisema kwamba ni watu wanaojuana na kwamba hawatoki Hollywood.

Kama wanaanga wa Apollo, wawili hao watasaifiri angani wakibeba matumaini na ndoto za binaadamu wote wanaopenda kusafiri.

Tunataraji kuwafanyia ukaguzi wa kiafya kabla ya kuanza kuwafunza baadaye mwaka huu.
Source: BBC

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.