Header Ads

Breaking News
recent

Baada ya tuzo za Grammy kumalizika mpiga gitaa maarufu duniani amchana Beyonce kuwa sio muimbaji.

Mpiga gitaa maarufu sana duniani Carlos Santana ameamua kumchana Beyonce baada ya tuzo za Grammy kumalizika.

Baada ya Adele kunyakua tuzo kubwa za Grammy ikiwemo Album ya Mwaka aliyokuwa akishindana na Beyonce, Santana amesema Queen Bey alikosa sababu sio muimbaji.

 “Nadhani Adele alishinda kwasababu anaweza kuimba,” aliimbia Australian Associated Press

“Kwa heshima na taadhima kwa dada yangu Beyoncé, Beyoncé ni mzuri sana kumwangalia ni kama muziki wa ulimbwende, sio muimbaji,” aliongeza.
 “Adele anaweza kuimba. Haleti dancers wote, huweza kusimama tu pale na kuimba wimbo na hivyo tu, na ndio maana anashinda.”

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.