Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

January 17, 2017

WHO yazitaka nchi za Afrika kuimarisha mifumo ya kitaifa ya usalama wa chakula

Shirika la Afya Duniani WHO limezitaka nchi za Afrika kuimarisha mifumo ya kitaifa ya usalama wa chakula, ili kuboresha afya ya wananchi wao. 

 Kwenye kongamano la 22 la kamati ya uratibu ya CODEX barani Afrika, mjumbe wa shirika hilo nchini Kenya Bw. Rudi Eggers amesema, licha ya kuwa nchi nyingi za Afrika ziko katika vipindi tofauti vya kuimarisha mfumo wa usalama wa chakula, juhudi zaidi zinahitajika. Bw Eggers amesema kuimarisha mifumo ya usalama wa chakula ni muhimu kwa Afrika na ni kipaumbele kwa WHO.
Source: CRI