Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

January 21, 2017

Wana mazingira wazitaka serikali za nchi za Afrika kuwekeza kwenye nishati endelevu

Wanamazingira barani Afrika wamezitaka serikali za nchi za Afrika kuwekeza zaidi kwenye miradi ya nishati endelevu, ili kuhakikisha bara la Afrika linakuwa na siku za baadaye zenye neema na zisizo na uchafuzi.

Wakiongea mjini Nairobi kwenye kongamano la ngazi ya juu kuhusu sera, wanamazingira wamezitaka nchi za Afrika kuweka sera na hatua za motisha ili kuhimiza uwekezaji kwenye nishati endelevu.

Katibu mkuu wa jumuiya ya haki kwenye masuala ya hali ya hewa mjini Nairobi Bw. Mithika Mwenda, amesema kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati ya visukuku kwenda kwenye matumizi ya nishati endelevu, ni muhimu kwa Afrika kukabiliana na changamoto za kimazingira na kiuchumi.

Credit: CRI