Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

TAZAMA KIONJO CHA JIBAMBEE TV SHOW

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

January 14, 2017

Uchumi wa Zimbabwe waongezeka kwa asilimia 0.4 mwaka jana

Benki ya Dunia imesema kutokana na athari ya ukame, na kupunguza matumizi ya jumla ya fedha, ongezeko la uchumi la Zimbabwe kwa mwaka 2016 liliongezeka kwa asilimia 0.4 tu, ambalo ni la chini zaidi kuanzia mwaka 2009.

Ripoti iliyotolewa na Benki hiyo katika kipindi kipya cha mustakabali wa uchumi wa dunia imekadiria kuwa, uchumi wa Zimbabwe utaongezeka kwa asilimia 3.8 mwaka huu, lakini serikali ya Zimbabwe ilikadiria kuwa uchumi wake utaongezeka kwa asilimia 1.7 tu.