Header Ads

Breaking News
recent

Top 20 ya miji duniani inayotumia baskeli zaidi kuliko magari.

Kwa hapa Tanzania baadhi ya miji ambayo usafiri wa baiskeli ni mkubwa zaidi kuliko Magari ni pamoja na Shinyanga ambako Baiskeli zimepewa jina la ‘daladala’ na ndizo zinazofanya safari za hapa na pale na kukupeleka mpaka mlangoni.

Sasa katika rekodi za dunia utafiti uliofanywa ulionyesha kwamba kuna miji mingi duniani ambako Baiskeli ndio suluhisho la watu kuwahi zaidi wanakokwenda kuliko kutumia magari ambayo yanakwamishwa na foleni au mizunguko.

Miji yenyewe ni Copenhagen, Amsterdam, Utrecht, Strasbourg, Eindhoven, Malmo, Nantes, Bordeaux, Antwerp, Seville, Barcelona, Berlin, Ljubljana, Buenos Aires, Dublin, Vienna, Paris, Minneapolis, Hamburg na Montreal.

Mji wa Copenhagen Denmark umeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya baiskeli ambazo huingia katikati ya jiji kila siku ukilinganisha na magari.

Unaambiwa mwaka 2015 magari 252,600 yalitumiwa kwenye jiji hilo ikilinganishwa na baiskeli 265,700 ambazo zilionekana kwenye mitaa ya jiji hilo ambapo ripoti ya utafiti huo imeeleza kuwa ni mara ya kwanza takwimu kueleza hivyo tangu mamlaka husika zianze kuhesabu mwaka 1970.

Source: millardayo.com

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.