Header Ads

Breaking News
recent

Sayansi na Teknolojia: Wanasayansi wagundua waya wa umeme mwembamba zaidi.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani wametoa ripoti kwenye gazeti la Nature Materials la Uingereza ikisema wametengeneza waya mwembamba zaidi wa umeme wenye kipenyo cha atomu 3 tu kwa almasi.

Kama tunavyojua, almasi inaundwa na atomu za kaboni. Muundo wa almasi ni kwamba kila atomu ya kaboni inaungana na atomu nyingine 4, na muundo huo unaifanya almasi iwe ngumu sana. 


Watafiti wametengeneza almasi ndogo sana yenye atomu 10 tu za kaboni, halafu wameiunganisha almasi hii na atomu ya sulfur na atomu ya shaba. 


Atomu hizi 12 zinaunda kipande kimoja cha waya. Kwenye majimaji maalum, vipande hivi vinajikusanya pamoja vyenyewe na kuunda waya. Atomu za sulfur na shaba zilizoko ndani zinapitisha umeme, na atomu za kaboni zilizoko nje zinakuwa safu ya kuhami.

Watafiti wamefahamisha kuwa waya huo wenye kipenyo cha atomu 3 tu unaweza kutumiwa kutengeneza vipuri vidogo vyenye urefu wa nanomita kadhaa au vipuri vinavyozalisha umeme kwa nishati ya jua.


 Na wakibadilisha atomu ya shaba kuwa atomu za cadmium, zinc, chuma au fedha, wataweza kutengeneza nyaya zenye sifa mbalimbali.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.