Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

January 10, 2017

Madhara ya dawa pale unapokuwa mnywaji wa pombe kupitiliza..

Unywaji wa pombe uliopitiliza huongeza hatari ya kupata homa ya ini (Athari mbaya za dawa kwa ini) pale unapotumia dawa aina ya Acetaminophen maarufu kama Paracetamol au Panadol.

 Hii ni kwa sababu unywaji wa pombe hupunguza akiba ya “Glutathione” mwilini kemikali inayolinda chembe hai za ini.

 Ili acetaminophen itolewe mwilini haina budi kuvunjwa vunjwa na ini ilikupata kemikali ambayo itatolewa mwilini kupitia mkojo pale utakapokojoa.

Moja wapo ya zao la kuvunjwa vunjwa kwa acetaminophen ni N-acetylbenzoiminoquinone ambayo inatakiwa kuungana na Glutathione lasivyo itaungana na seli /chembe hai za ini na kuziharibu na kupelekea homa ya ini. ENDELEA HAPA