Header Ads

Breaking News
recent

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Airtel nchini Kenya kufanyia majaribio intaneti ya 4G wiki ijayo .

Kampuni hiyo imesema awamu yake ya kwanza itakuwa kwenye maeneo 40 katika mji mkuu Nairobi kabla ya kuenea kwenye maeneo mengine 45 katika miji mikubwa kama vile Mombasa na Kisumu ifikapo mwezi Machi.

Airtel itahitajika kupata leseni kutoka kwa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya kwa gharama ya shilingi bilioni 2.5 kabla ya kuanza huduma hiyo.

Tayari kampuni ya Safaricom imeanza huduma za 4G kwenye miji kadhaa ikiwemo Nakuru, Eldoret, Meru, Kisii, Kisumu, Mombasa na Kisumu.

Mgao wa soko wa Airtel uliimarika miezi tatu iliopita kwa 0.9 na kufikia asilimia 17.5.

Source: CRI

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.