Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

January 4, 2017

Janet Jackson ajifungua mtoto wa kiume katika umri wa miaka 50.

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Janet Jackson amejifungua mtoto wa kiume akiwa na umri wa miaka 50, afisa wake wa mawasiliano amethibitisha.

Taarifa imesema mwanamuziki huyo na mumewe Wissam Al Mana, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Qatar, wana furaha kumpata mtoto wa kiume kwa jina Eissa Al Mana.

"Janet alijifungua bila matatizo yoyote na kwa sasa anapumzika," afisa wake amesema.