Header Ads

Breaking News
recent

Drake, Kanye West, Justin Bieber na Frank Ocean hawatahudhuria tuzo za Grammy 2017.

Tuzo za Grammy ni tuzo kubwa sana za wasanii duniani kote zinazofanyika kila mwaka nchini Marekani
Inasemekana baadhi ya wasanii wakubwa nchini humo hawatahudhulia tuzo hizo na miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Drake, Kanye West, Justin Bieber, na Frank Ocean.

Sababu za kuto kuhushuria sherehe hizo za 59 ni....

Ocean ambaye aliyeachia Album yake mwaka jana "Blonde and Endless" alishindwa kuwasilisha uwepo wake katika tuzo hizo."Inaonyesha kuwa haiwakilishi vyema watu wa eneo langu ninapotoka na kile nilicho nacho".

 Kanye West ameteuliwa katika vipengele nane na hadi hapo tayari alikwisha twaa tuzo 21 Grammys katika kipindi kilichopita, lakini bado ameonekana kuitelekeza tuzo ya mwaka huu. 

Mwezi October, alinukuliwa akisema, “If [Frank’s] album’s not nominated in no categories, I’m not showin’ up to the Grammys.” "Kama Album ya Frank aichaguliwa kuingia katika kipengele chochote, basi sitaonekana katika tuzo za Grammy".

Japokuwa anatuzo nane za Grammy, Drake mwaka huu atohudhuria sherehe ya tuzo hizo, kutokana kuwa atakuwa katika Boy Meets World Tour" yake”.

Justin Bieber, ambaye amechaguliwa kuingia katika kipengele cha Album Bora ya Mwaka, naye hatohudhuria katika sherehe hizo za utoaji tuzo.

Hii ni kwamujibu wa TMZ, ambao pia wamesema "wasanii wanahisi kuwa tuzo za Grammy mwaka huu hazina mvuto". 

Hata hivyo, sherehe hizo za Grammy zitafanyika kama kawaida. Sherehe za 59th Annual Grammy Awards zitafanyika Feb. 12 huku baadhi ya wasanii watakaotoa burudani wakiwa ni Adele, Bruno Mars, na John Legend, na wengineo...

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.