Apotea njia na kujikuta akiendesha baiskeli siku 30 China.
Mwanamume mmoja nchini China ambaye
alikuwa na matumaini ya kuendesha baiskeli hadi nyumbani kwao
kusherehekea mwaka mpya, aligundua baada ya siku 30 kuwa alikuwa
amepotea njia.
Lakini alisimamishwa na polisi wa trafiki akiwa amepotea umbali wa kilomita 500 katika mkoa wa Anhui.
Wakati waligundua, polisi walimlipia tikiti ya treni ili arudi nyumbani.
Ripoti zinasema kwa mwanamume huyo alikuwa akilala maduka ya intaneti kwa sababu hakuwa na pesa.
Mwanamume huyo hakuwa na uwezo wa kusoma ramani na hivyo alikuwa akitegemea watu kumuelekeza.
Polisi walimsimamisha kwa sababu alikuwa akitumia barabara ambayo baiskeli haziruhisiwi kuitumia.
Baada ya kugundua makosa yake, polisi na watu wote waliokuwa kituoni ambapo alisimama walichanga pesa na kumnunulia tikiti ili asafiri nyumbani.
Credit: BBC swahili
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA