Header Ads

Breaking News
recent

Vitu 10 Amazing kuhusu Tanzania.

Tanzania ni Muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar na inakadiriwa kuwa na takribani zaidi watu milioni 45 ambao ni raia wake.
Tanzania imekuwa ni kitovu cha utalii (mbuga za wanyama ) Afrika, huku ikikupa wakati mzuri wa kufurahia hali ya hewa, milima na mabonde uwapo Tanzania.

Hapa nakusogezea vitu vitano (5) ambavyo huenda hukuwa unavifahamu:-

1. Karibia 30% ya Tanzania ni Mbuga za wanyama za Taifa, huku hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikitajwa kuingia katika maajabu 7 ya dunia.

2. Mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu Barani Afrika na wenye urefu wa mita 5,895 juu ya usawa wa bahari.
3. Takribani wanyama milioni 2 (Nyumbu) husafiri katika maeneo tambalale.

4.Ngorongoro Crater ni moja ya maeneo bora kabisa kwa kuangalia Big Five (Simba, Tembo, Faru n.k) ambayo pia ilitajwa kuwa ni moja ya maajabu saba asilia Afrika.

5. Ziwa Tanganyika ni Ziwa la pili kwa ukubwa duniani, huku likiwa na takribani viumbe maji 500 wanaopatikana katika ziwa hilo.

6. Miti ya Mibuyu inayopatikana pia katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire, inasemekana inauwezo wa kuishi hata zaidi ya mika 1,000, japo mti mkongwe kabisa wa Mbuyu uliosadikika kuishi kwa muda wa miaka 6,000 huko Afrika ya Kusini. 

7. Tanzania yetu ni ya watu wakarimu na wanaopenda kupiga stori sana hasa kwa wageni waingiao nchini.

8. Madini ya Tanzanite yanapatikana tu Tanzania, kaskazini mwa Tanzania. 

9. Gesi ni sehemu ya nishati iliyogunduliwa hapa Tanzania na tayari ilishaanza kufanyiwa kazi.

10. Tamaduni, mila na desturi zetu ikiwa ni pamoja na chakula, burudani na lugha ya Kiswahili ni vitu vinavyowavutia wengi wanaoitembelea Tanzania.

Hayo pamoja na mengine mengi ndiyo yanayo ifanya asili ya mtanzania iwe tofauti na nchi nyingine. Asanteni sana na karibu tena.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.