Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

TAZAMA KIONJO CHA JIBAMBEE TV SHOW

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

December 9, 2016

Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mengi yapo.

Ni Desemba 9 2016 ambapo Tanzania Bara inaadhimisha Miaka 55 ya Uhuru huku Srikali ikipambana na kutokomeza Rushwa na Ufisadi.

Akizungumza leo katika sherehe za uhuru jijini Dar es Salam, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli ameeleza kuwa, katika mwaka ujao sherehe kama hizo zitaanza rasmi kufanyika katika mji mkuu wa Tanzania Dodoma na sio Dar es Salaam tena.

Katika serikali ya awamu ya Tano imeonesha juhudi zake za kupambana na Rushwa, Ufisadi na kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya Taifa letu, hivyo wananchi ni vyema  tukaunga mkono Serikali katika mapambano haya.