Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

November 7, 2016

Samwel Sitta Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania afariki dunia.

Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Samuel Sitta mwezi Septemba, 2016.
Spika wa zamani wa bunge la Tanzania Samwel Sitta amefariki dunia akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.
Sitta alikuwa mbunge mstaafu wa jimbo la Urambo lililopo mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu, Bw Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.

Amekuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.
Rais wa Tanzania John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kusema amepokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha spika huyo.

Sitta alikuwa Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na alikuwa pia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina