Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

October 26, 2016

Video: Diamond Platnumz aonesha video fupi ya nyumba yake mpya ya Afrika ya Kusini.

Siku kadhaa zimepita toka msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz atangaze kuwa kanunua nyumba ya kuishi Afrika Kusini.

Baada ya kutangaza kununua nyumba hiyo iliyomgharimu zaidi ya shilingi milioni 400, maneno mengi yalisemwa yakiwemo ya wale waliohisi amepiga changa la macho. Na sasa muimbaji huyo amethibitisha kuwa mjengo huo ni mali yake baada ya kuwasili rasmi Jumanne hii. 

Akiwa na timu yake ya WCB, Diamond ameikagua nyumba kwa mara ya kwanza na kuwasogeza karibu nayo mashabiki wake kwa video alizoweka Instagram.