TEMBELEA BLOG HII KILA UPATAPO MUDA, ITAKUFUNGUA KATIKA FURSA NA STADI ZA MAISHA

Latest Articles

October 24, 2016

Msanii wa rap maarufu kama Drake ambaye pia juzi kati alichukua headline kupitia album yake mpya kwa kusikilizwa sana katika mtandao wa Apple Music, leo amesherehekea siku yake ya kuzalia.

Drake ametimiza miaka 30, ambapo kwa mujibu wa TMZ staa huyu alipewa kampani ya nguvu na mastaa wengine kama vile, Taylor Swift, Katy Perry, John Mayer, French Montana, na Jamie Foxx.


Drake hakuishia kula tu keki, ni siku chache alipotangaza project mpya 'More Life' pia ameachia ngoma nne kwa mpigo, ”Two Birds, One Stone,” the London On Da Track-produced “Sneakin'” featuring 21 Savage, and “Fake Love” (produced by Vinylz and Frank Dukes).
Continue reading

Rapper J. Cole amefanikiwa kupata double platinum kwa kuuza kopi zaidi ya milioni 2 za album yake, 2014 Forest Hills Drive bila collabo yoyote, hii ikiwa ni kwa mujibu wa Recording Industry Association of America.
Continue reading

Filamu ya ‘Brother Jekwu’ aliyoshirikishwa mwanamitindo wa Kenya, Huddah Monroe inatarajiwa kuanza kuonekana kwa mara ya kwanza Disemba 2, mwaka huu.
‘Brother Jekwu’ ni filamu ya muigizaji mkongwe wa Nigeria, Mike Ezuruonye iliyofanyika nchini Nigeria huku ndani yake akiwashirikisha mastaa kadhaa akiwemo Candy, Angela Okorie, Miss Kenya 2004 na wengine.
Filamu hiyo ilianza kutengenezwa mwezi April, mwaka huu na itakuwa ni filamu ya kwanza kwa Huddah kuigiza.
Credit: Bongo 5
Continue reading

Stori zinatoka kwa Justin Bieber wakwetu, hii ni baada ya kuondoka katika jukwaa la tamasha lake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki kutopiga kelele wakati anapoimba.

Wakati wa matamasha yake matatu yalizopita katika mji huo ikiwa ni  miongoni mwa ziara yake ya dunia nzima, mwanamuziki huyo alisema : "Nathamini msaada ninaopata, nathamini mapenzi mnayonipa na nathamini ukarimu wenu. Lakini kelele mnazopiga wakati ninapoimba lazima zisitishwe.Tafadhali na ahsanteni.Sidhani ni muhimu ninapojaribu kusema kitu na nyinyi mnapiga kelele.

Kwa upande wa mashabiki walipokataa kusitisha kelele zao, Bieber aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa, huku baadhi ya mashabiki wakimzomea.

Baadaye mkali huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha lake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.
''Nahisi kwamba nataka kuwasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho, mnajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana''.
Continue reading

Ni october 24 2016 ambapo Hit Maker wa ngoma ya "Please Don’t go Away" Mayunga ameelezea alivyokwenda Marekani kurekodi na Staa Akon, Mayunga ameweka wazi siku aliyopewa mdundo wa Please dont go Away, time ikiwa imekata yani siku moja tuu kabla ya kurekodi. Basi mpimie hapo chini.... 
Credit (Millardayo)

Continue reading

Will Smith (kulia) akiwa na mwanae Jaden.
Baba na mwana.

Jada Pinkett Smith

Continue reading

Yule mkali wa miondoko ya R&B kutoka Marekani, maarufukama Joe Thomas akimshirikisha rapa Gucci Mane wamekuletea single hii “Happy Hour.”
Continue reading

October 23, 2016


Story zinaandikwa kutoka nchini Misri kuhusu Mwanamke mnene kuliko wote duniani, ambaye anatajwa kufikisha uzito wa kilo 500.

Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo 500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia ukuaji wa mwili.

Akiwa na miaka 11 alianza kusumbuliwa na tatizo hilo ingawa wazazi wake wanakiri kuwa hawakudhani kuwa ni tatizo lakini siku zilivyozidi kwenda ndipo wakabaini kuwa halikua jambo la kawaida hivyo wakaamua kutafuta wataalamu ambao walitoa ripoti kuwa ana matatizo ya mwili wake kukaa na maji mengi bila kuyatoa nje kitu ambacho sio cha kawaida kwa binadamu.
Source: TZA
Continue reading

October 19, 2016Ulaji wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.

(1)Husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa na asili ya nyuzi nyuzi au, fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito hivyo kuzuia magonjwa mbalimbali.

(2)Hupunguza (hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa na hangovers.

(3) Husaidia katika mmeng'enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.

(4) Husaidia kuondoa msongo wa mawazo kwani yana kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.

(5) Husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini c.

(6) husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.

(7) Husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni..

(8) Husaidia mtu kupata choo laini na huzuia kukosa choo.
(
9) Huzuia kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu ili kuwezesha mzunguko sahihi wa damu kaitika pande zote za mwili sambamba na kurekebisha mapigo ya moyo.

(10) Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.
 Source: Mo Blog
Continue reading

October 18, 2016

Leo, Oktoba 18, ni miaka 9 tangu mwanamuziki wa nyota wa reggae wa Afrika Kusini, Lucky Dube auawe kwa kupigwa na risasi.

Kwa heshima ya mwanamuziki huyo, waziri wa sanaa na utamaduni, Nathi Mthethwa amelitaka taifa hilo lisherehekee mchango wake kwenye muziki.

“Today we pay tribute to Raggae music icon Lucky Dube who died tragically on this day in 2007. His music touched millions across the globe,” ameandika kwenye Twitter.


Oktoba 18, 2007, Lucky Dube aliuawa kwenye kitongoji cha Rosettenville jijini Johannesburg, muda mfupi baada ya kuwashusha watoto wake wawili kati ya saba kwenye nyumba ya mjomba wao.

Polisi wanasema watu waliomuua hawakujua kama nini yeye na walidhani ni Mnaijeria. Watu watano walikamatwa na watatu walipatikana na hatia na kuhukumiwa March 31 2009. 

Wawili kati yao walijaribu kutoroka na walikamatwa. Walihukumiwa kifungo cha maisha jela.

Source: Bongo5
Continue reading

October 2, 2016

Leo wakali kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 Baraka The Prince na Alikiba wameachia ngoma mpya ya video ambayo ni ya Baraka Da Prince inayoitwa "Nisamee".

Continue reading

August 26, 2016

Hii ni gari aina ya Mercedes F015 ambayo imetengenezwa na wajerumani, kampuni ya the house of German Mercedes yenye uwezo wa kujiendesha yenyewe bila dereva.


Gari hii ina uwezo wa kuhisi pale ambapo kitu chochote au mtu anapita mbele yake na likasimama lina uwezo wa kutumia sauti kama njia ya kumpa mtu taarifa, siti za mbele zina uwezo wa kuzunguka na kugeukia upande wa nyuma endapo watu watajisikia kupiga story kwa kuangaliana.
Gari hiyo itazinduliwa rasmi na kuanza kuuzwa kwa matumizi binafsi kama magari mengine rasmi mwaka 2017.
Tazama video hii hapo chini.....

Continue reading

August 25, 2016

Baada ya stori ya kumpatia zawadi ya gari Raymond kutawala media, mengine yameibuka mapya na makubwa zaidi baada ya hitmaker huyo wa Kidogo kuonekana akiwa na staa wa Nigeria, Wizkid huku mashabiki wakijiuliza nini kinaendelea?

Tazama video hii hapa....

Tazama na hii....

Continue reading

Ndege ndefu zaidi duniani - Airlander 10 - imeharibika baada ya kuanguka ikitua kwenye safari yake ya pili ya kufanyiwa majaribio.
Ndege hiyo ya urefu wa 302ft (92m) - ambayo kwa kiasi fulani ni ndege na pia kwa kiasi fulani puto - iliharibika ikiwa katika uwanja wa Cardington, Bedfordshire nchini Uingereza.
Ndege hiyo ya thamani ya £25m imeharibika eneo wanamoketi marubani baada ya kuangika kwa 'pua' mwendo wa saa tano saa za Uingereza.

Airlander 10 kwa takwimu
  • 44,100 lbs (20,000kg): Uzani wa ndege hiyo
  • 20,000ft (6,100m): Umbali ambao inaweza kupaa juu angani
  • 80 knots (148km/h): Kasi yake ya juu zaidi
  • Siku 5: Muda ambao inaweza kukaa angani
  • 22,050 lbs (10,000kg): Uzani ambao inaweza kubeba
Chanzo:BBC

Continue reading