UTANI.COM
Traffic Zuzu alimsimamisha mwanamama aliyekua anaendesha
gari mitaa flani hivi.
Traffic: Naomba Leseni yako tafadhali.
Mwanamama: Leseni ndo ikoje?
Traffic: Ina shepu ya mstatili afu ina sura yako. Mwanamama
akapekua mkoba wake akatoa kioo cha kujirembea akampa afande.
Traffic: (Baada ya kuitazama) Kama ungeniambia mapema kuwa
wewe ni Traffick nisingekusimami sha, uwe unasema!
Na John Mushi
JUHA, ZUZU NA ZOBA
Juha-Nilimpigia cm mke wangu akapokea, Hakusema hallow nikauchuna
sikuongea mpaka pesa zote zikaisha
Zoba-Niligonga mlangomke wangu akafungua hakuniambia karibu
nikasimama palepale mlangon mpaka kesho.
Zuzu-Tangu nimuoe mke wangu hajaniita Mpenz nimegoma kulala nae
hadi leo ni miaka 6.
Wote wakamwambia Wee mwongo mbona unawatoto 2 ?
Zuzu-akajibu mpaka leo sijamuuliza watoto ni wa nan?
Nimeuchuna tu.......!
Na.. John Mushi
*************************************************************************************
JAMAA ALIMPENDA DEMU KANISANI
Huu mgentloman mwingine ni extraodinary jamaa
kamzimia mrembo kanisani,
mara ukafika mda wa
sadaka,eti akamwambia
"dont worry i'll pay for u"!!
Na John Mushi ************************************************************************************
DEREVA TAX NA JAMAA FLANI ALIYEKUWA ANAUMWA
Jamaa alikuwa anaumwa akapita kituo cha taxi akaikuta taxi moja, akamuomba sana taxi dreva ampeleke hospitaji lakini fedha yake ilikuwa ndogo, kitu cha ajabu dreva alimporomoshea jamaa matusi ya nguoni na kumwambia akapande bodaboda kama hana hela. Wiki mbili baadae jamaa akawa amepona na anapesa mkononi, akaenda kituo cha taxi akakuta taxi nne ikiwemo ya yule dreva aliyewahi kumtukana, akamwendea dereva wa kwanza; JAMAA: Natafuta dereva wa taxi shoga niondoke nae ntamlipa laki DEREVA 1: We mwenda wazimu nini hebu toka hapa.. Jamaa akenda taxi yapili JAMAA: Natafuta dereva shoga niondoke nae ntamlipa laki DEREVA 2: Pumbavu mkubwa toka hapa. Hatimae jamaa akaenda kwa yule taxi dreva aliyewahi kumtukana JAMAA: Aise sijui unaweza kunipeleka Ubungo? DEREVA: Ndio shilingi alfu kumi JAMAA: Haya twende....wakati wanaondoka jamaa akahakikisha anapungia mkono wale madereva waliobaki kituoni huku akionyesha alama ya kidole gumba. Akiwaacha midomo wazi..
Na mwana vituko wetu- John Mushi
*************************************************************************************
SWAGA ZA ASKARI POLISI ANAPOMTONGOZA DEMU.
Heh! tulipata swaga za ticha wa physics ktk harakat za kumtokea dem xaxa daka hii........ Swaga za polisi anapofukuzia demu, Unajua nakuthamini zaidi ya rushwa na posho, bira ya wewe mimi siwezi kuishi, ni sawa na kukosa bunduki eneo ra tukio,nakuheshimu kama ninavyoheshimu rindo, wewe ndio IGP wa moyo wangu. Mbona upo kimya, nina RB ya penzi rako, nijibu nifungue jarada rako ndani ya moyo wangu. Usifanye moyo wangu ukaenda mbio kama difenda mpya,.Nakuhakikishia nitakuwekea usarama kama msafara wa Rais, usiniweke roho juu kama maandamano ya CHADEMA nijibu poti.
Kwa hisani ya John Mushi - Mo Town. .......................................................................................................................................................................
WIFE!
As soon as I get through with you, you'll have a clear case for divorce and so will my wife.
Mtu na mkewe wanagombana chumbani, ghafla ugomvi unakuwa mkubwa mke anaamua kukusanya vitu vyake kwa lengo la kuondoka. Mume anashangaa anamuulizaa: Unakusanya vitu unaenda wapi? Mke kwa nyodo anajibu: Nakwenda kwa mama yangu. Mume naye akaanza kukusanya nguo zake na kuweka kwenye mabegi yake, mke kwa jeuri akamuuliza mume wake: Unapaki unakwenda wapi? Mume akajibu kwa tabasamu: na mimi nakwenda kwa mama yangu. Mke akauliza tena "Hawa watoto wako watabaki na nani?
![]() |
- Demu wako ni mwembamba hadi akivaa tshrt ya blue anafanana na sim card ya tigo.Unapenda hela hadi ukiulizwa muda unajibu oooh!! saa mbili "CASH"