Header Ads

Breaking News
recent

Utafiti mpya kuhusu siafu na utendaji kazi wao.

Utafiti mpya wa Marekani umeonesha kuwa jeni inayohusiana na uwezo wa kuhisi harufu ni muhimu sana kwa vitendo vya siafu waishio kijamaa, na kama jeni hii ikibadilika, siafu watapoteza uwezo wa kuwasiliana, kutafuta chakula na kuzaliana.

Siafu ni wadudu waishio kijamaa, wanawasiliana na kushirikiana kwa kutoa na kuhisi harufu maalum.


Watafiti wa Chuo Kikuu cha New York wametoa ripoti kwenye gazeti la Cell la Marekani wakisema baada ya kurekebisha jeni ya Orco ya siafu aina ya Harpegnathos saltator, uwezo wa kuhisi harufu wa siafu hao ulipungua kwa kiasi kikubwa, na kusababisha siafu hao kupoteza uwezo wa kuwasiliana na wenzi wao, kurudi nyumbani kwa kufuata harufu, na kutafuta chakula.


Mabadiliko ya jeni hiyo pia yanaathiri vibaya kitendo cha kuzaliana cha siafu jike. Kwenye kundi la siafu hao, baadhi ya siafu wafanyakazi wana uwezo wa kugombea hadhi ya umalkia. 


Wakati malkia anapokuwa hai, harufu yake inawazuia siafu wafanyakazi kugombea hadhi hiyo, lakini akifa, siafu hao wanaanza kupambana, na mshindi anakuwa malkia mpya na kubeba jukumu la kuzaliana. 

Siafu mwenye jeni iliyobadilika hawezi kupambana na kuzaliana kama kawaida, hata akitaga mayai, hayatunzwi na siafu wadogo mara kwa mara, hivyo ni vigumu kwake kupata watoto.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.