Header Ads

Breaking News
recent

Wayney Rooney aikacha Manchester United na kujiunga na Everton.

Mchezaji wa kitambo wa Timu ya Man United na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney amekata mzizi wa tetesi baada ya kusajiliwa na klabu mpya.

Kupitia mtandao wa klabu ya Everton taarifa zimesema wamefikia makubaliano hayo kwa mazungumzo ya muda mrefu na baada ya kutathmini uwezo wake na umri pamoja na uzalendo wake kwa klabu hiyo ambayo ndiyo imemkuza tangia akiwa na mika nane kabla ya kununuliwa na Man united mwaka 2004.

Tayari Rooney amekubali kujiunga na Everton kwa kupunguza mshahara wake wa wiki kutoka paundi 250,000 anazolipwa sasa na Manchester United mpaka 180,000 kiasi ambacho Everton wamekiri kukimudu.

Rooney kukubali kujiunga na Everton basi tumtegemee kujipatia tiketi ya kutembelea Tanzania kuja kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia alhamisi ya wiki lijalo (tarehe 13 julai).

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.