Header Ads

Breaking News
recent

Top 10 ya wanamichezo wa kiume matajiri zaidi duniani kwa mwaka 2017

10. RAFAEL NADAL- $125 million
Huyu ni staa namba moja wa mchezo wa tenesi, ameshinda tuzo nyingi duniani, na unaambiwa kila mechi anayocheza analipwa sii chini ya dola milioni 4.5 na unaweza kumuita kama “The King Of Clay”.

9. Phil Mickelson- $180 million
Huyu ni staa wa mchezo wa Golf kutoka Marekani, amezaliwa June 16. 1970 huko California. Na amekwisha shinda championships 43 za PGA Tour na nyingine kibao.
8. Lionel Messi - $218 million 
Alizaliwa 24th June 1987. Ni staa wa mpira wa miguu kutoka Argentina na mchezaji nyota wa soka wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.
Messi amekwisha shinda tuzo mara 3 ya Kiatu cha dhahabu Ulaya. Huku Barcelona akishinda tuzo 8 za La Liga na 4 UEFA Champions League.
7. Manny Pacquiao- $250 million
Huyu ni staa wa ngumi kutoka Ufilipino, alizaliwa 17 December 1978 huko Kibawe, Bukid-non, Ufilipino
Pac anatajwa kuwa ni bondia mzuri zaidi kuwahi kutokea na ambaye ameshinda tuzo 9 za dunia.
Manny Pac anafahamika kama mtaalam wa ngumi anayechuana na mkali Floyd Mayweather katika mchezo wa ngumi.
6. Cristiano Ronaldo- $280 million
Huyu ni staa wa soka duniani kutoka Ureno, alizaliwa 5 February 1985.
Na ni mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno. Ni mchezaji pekee aliyewahi kushinda tuzo 4 za European Golden shoes.
Na mwaka 2009 aliondoka Manchester United na kuhamia Real Madrid kwa dau la $132 million.
5. LeBron James- $300 million
Huyu ni staa wa mchezo wa kikapu kutoka Marekani, ana urefu wa futi 6, LeBron James ni Mmarekani mweusi anayeichezea timu ya kikapu ya Cleveland Caval-ries
Alizaliwa 30th December 1984 huko Akron. James ameshinda tuzo 3 za NBA Champion titles, na 4 za NBA kama Mchezaji Muhimu zaidi, 12 za NBA All-Star title, 2 za Mr. Basketball USA na nyinginezo. Alianza kucheza kikapu toka akiwa sekondari.
4. Roger Federer $320 million 
Huyu ni staa wa mchezo wa tenesi, Roger Federer anatajwa kama mchezaji wa tenesi namba 3 duniani.
Alizaliwa 8 August 1981 huko Switzerland
Ameonyesha kushika nafasi ya Dunia ya 1 kwa wiki zaidi ya 300 na wiki 237 mfululizo. 
Federer ameshinda tuzo zaidi ya 88 katika kazi yake ya mchezo wa tenesi na nimchezaji pekee wa tenesi aliyewahi kushinda tuzo 5 za mashindano ya US Open mfululizo.
3. Kobe Bryant $320 million 
 Huyu ni staa maarufu duniani wa mchezo wa mpira wa kikapu, ni mchezaji mkubwa sana kutoka timu ya Los Angeles Lakers.
Kobe alizaliwa 23rd August 1978 huko Philadelphia, Marekani. Ameshinda tuzo 5 za NBA Champion, 2 za NBA finals Most Valuable Player au Mchezaji Muhimu zaidi, 18 za NBA All-Star na nyinginezo.
2. Floyd Mayweather $620 million 
Huyu ni staa wa masumbwi na mmarekani mweusi, anayetambulika kama mpiganaji ngumi bora kwa wakati wote. 
Floyd alizaliwa 24th February 1977 huko Michigan.
 Ni mshindi wa mataji 15 ya dunia na inasemekana kuwa ni bondia wa uzito wa juu kwa muda wote.
Amekuwa ni bondia ambaye ameshinda mataji 23 kwa Knockout nje ya mataji 49 aliyoshinda.
Mayweather anatajwa kutengeneza kodi/ushuru wa kiasi cha $1.3 billion katika kazi yake ya ngumi.
1. Tiger Woods- $700 million
Huyu ni nyota wa Golf duniani kwa muda murefu hadi sasa na anatajwa kuwa, ndiye mwana michezo anayeongoza kwa kuwa na mkwanja mrefu zaidi duniani.
Eldrick Tont maarufu kwa jina la ‘Tiger’ Woods ni Mmarekani na mcheza Golf maarufu anayetajwa kwa muda wote.
Amewahi kushinda tuzo ya PGA kama mchezaji bora wa mwaka. Tiger anatajwa kuwa mjezaji mdogo zaidi wa golf aliyekuja kwa kasi na kushinda tuzo 50 katika mashindano ya ziara. 
Tiger ametajwa kama mchezaji anyelipwa pesa nyingi zaidi duniani katika miaka mingi.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.