Header Ads

Breaking News
recent

Msanii Rihanna atoa msaada wa milioni za dola katika elimu nchini Malawi.

Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna  ametoa msaada  wa kiasi cha Us dola milioni 20 nchi  Malawi kwa ajili ya kusaidia miundombinu  katika sekta ya Elimu.

Rihanna na kwa kushirikiana na GPforEducation, mwezi wa kwanza mwaka huu alitembelea nchi hiyo kwa lengo la kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.

“My time in Malawi was so inspiring! Working with my @ClaraLionelFdn to improve the lives of students globally, alongside @GPforEducation… ”

Msanii huyo ameendelea kutumia muda wake pamoja na mali zake ili kuinua sekta ya elimu barani Afrika.

Tatizo la ukosefu wa miundominu haipo Tanzanzia pekee bali hata nchi zingine kwenye bara la Afrika.
Picha na video za msanii huyo zimeanza kusambaa kwa kasi siku ya jana zikumuonesha yupo Malawi.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.