Header Ads

Breaking News
recent

Mji wenye maisha ya juu zaidi duniani, unapatikana Afrika.

Tumezoea kuona na kusikia tafiti nyingi zikifanyika huku zikiiacha Afrika mikono mitupu, labda tu kwa zile tafiti za upande wa kushoto ndiko tunakowekwa.

Sasa nikujuze kuwa utafiti uliofanywa na Shirika la Takwimu za Gharama za Kuishi Duniani (Mercer) umeutaja mji mkuu wa Angola, Luanda kushika nafasi ya kwanza duniani kati ya miji yenye gharama kubwa zaidi za kuishi.
Takwimu hizi zimetolewa na shirika la Mercer ambalo lilifanya utafiti. Katika takwimu hizo miji ya Tokyo, Zurich na Singapore pia nayo inachukua nafasi tano za kwanza. 

Mji wa London ulishuka hadi nafasi ya 30 hasa kutokana na kushuka kwa thamani ya paundi.

Utafiti huo wa kila mwaka huangazia masuala kadha kando na gharama ya kukodi nyumba. Utafiti huo huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji, ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi, chakula na burudani.
Tazama nchi nyinginezo hapo chini>>>
 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.