Header Ads

Breaking News
recent

Video na Picha za wakati miili ya wanafunzi wa Lucky Vicent wakiagwa mjini Arusha.

Ilikua ni Mei 6, 2017 majira ya asubuhi ndipo taarifa zilipoanza kuenea mitandaoni kwa wingi na baadae radio zikatangaza kuwa, kuna gari aina ya costar iliyokuwa imebeba wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Lucky Vicent, iliyoko Mkoani Arusha kuwa imepata ajali na wanafunzi wamefariki.

Hata hivyo idadi sahihi ilikujakufahamika kuwa, wanafunzi waliopoteza maisha ni 29 na dereva pamoja na waalimu, jumla ikawa ni idadi ya watu 32 waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Hadi stori hii inachapishwa hapa, majeruhi wawili bado walikua wanapewa matibabu kutokana na hali mbaya waliyokuwa nayo, Mungu awaponye waweze kupona tena.

Kwamujibu wa mamlaka husika,Wanafunzi hao walipata ajali wakiwa wanaelekea Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema, ambao inasemekana hufanywa kila baada ya muda flani.

Taharuki ilizidi kutanda mitandaoni, mitaani, nchi nzima na hata nje ya nchi huku vyombo vikubwa duniani kama vile Yahoo, BBC n.k picha za tukio zikiendelea kusambaa kwingineko duniani. 

Ni simanzi iliyomtawala kila mtanzania kuendelea kuumizwa na tukio hili la kupoteza taifa la kesho kwa njia hii katili.
Viongozi wa serikali, chama na dini walihudhulia katika ibada ya kuwaaga marehemu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha, ambapo Mh.Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliongoza tukio hilo.
 Nae Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa alikwisha toa salamu za rambirambi mapema wa wafiwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, pia leo kupitia ukurasa wake wa twitter kayaandika haya kuhusu msiba huo.

‘Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha 1/2’- Rais Magufuli

Tumewapoteza mashujaa wetu ktk elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu, tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania‘- Rais Magufuli
Pichani ni Mh. Makamu wa Rais Samia Hassan, Mh. Waziri wa elimu Joyce Ndalichako, Mh. Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo na wauguzi, wakimjulia hali mmoja wa wanafunzi majeruhi wa ajali hospitalini hapo.
Hivi ndivyo ilivyokua leo Mei 8, 2017 katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Karume jijini Arusha wakati wa kuwaaga wanafunzi wa Lucky Vicent waliofariki Mei 6, 2017 kwa ajali ya basi walilokua wakisafiria kwenda Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema.

 Tazama hizi picha mbili hapo chini, ndivyo ajali ilivyokuwa....
Mungu awapumzishe wapendwa wetu mahali pema peponi, amen.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.