Header Ads

Breaking News
recent

Zimetajwa nchi 10 zinazoongoza kwa usafi wa mazingira duniani ingawa zina idadi kubwa ya watu.

Kuwa na mazingira masafi ni jambo jema katika afya ya mwanadamu, japo sii jambo rahisi tu sehemu ya watu wengi kuonekana safi, hii bado ni changamoto kwa nchi nyingi duniani. 

Sasa nakusogezea orodha ya nchi 10 zinazotajwa kuwa na mazingira masafi licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, orodha hii ni kwa mujibu wa Environmental Performance Index .

10: Norway
Norway ni nchi ya kumi kwa kuwa na mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na mazingira machafu kwa zaidi ya asilimia 78.04

9: Sweden
Sweden inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na uchafu kwa zaidi ya asilimia 78.9

8: Austria
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zenye amani duniani Austria inatajwa pia kuwa moja ya nchi yenye mazingira safi na imeshika nafasi ya 8 kwa mwaka 2017.

7: Spain 
Kwa mujibu wa Environmental Performance Index Spain imeshika namba saba kati ya nchi zenye mazingira masafi ambapo imeweza kupambana na uchafu kwa zaidi ya asilimia 79.79

6: Germany
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi inazotembelewa kwa wingi lakini hii haifanyi ujerumani kuwa nchi chafu,kwani mwaka 2017 imeweza kushika nafasi ya sita miongoni mwa nchi safi zaidi duniani.

5: Czech Republic
Czech Republic imeshika namba tano kati ya nchi zenye mazingira safi kwa mwaka 2017 kwa mujibu wa ripoti ya Environmental Performance index .

4: Singapore 
Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zinazotajwa kama kitovu cha biashara duniani Singapore pia ni moja kati ya nchi yenye mazingira masafi ambapo imeweza kupamba na uchafu kwa zaidi ya asilimia 81.78.

3: Australia
Australia imeshika namba tatu kwa nchi zenye mazingira masafi kwa mwaka 2017 na kwa mujibu wa Environmental Performance index Australia imeweza kupambana na mazingira machafu kwa asilimia 82.4.

2: Luxembourg
Environmental Performance imeipa Luxembourg asilimia 83.29  na kuifanya kuwa nchi ya pili kwa mwaka 2017 kuwa na mazingira masafi duniani.

1: Switzerland 
Switzerland ni miongoni mwa nchi zenye mazingira masafi duniani ambapo wameweza kupambana na mazingira machafu kwa zaidi ya asilimia 87.67 ,kwa mujibu wa Environmental Performance Index Switzerland  ni miongoni mwa nchi zenye hewa safi.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.