Header Ads

Breaking News
recent

Diamond baada ya kuzindua perfume yake ya "Chibu Perfume" Waziri aeleza yake mpya ya moyoni.

Siku chache zimepita toka staa wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnumz kuzindua Perfume yake mpya inayoitwa “Chibu Perfume” na kuonesha kupokelewa kwa nguvu kubwa nchini Tanzania.

Hatahivyo ubunifu wa wa msanii Diamond umemfikia Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangalla na kumfanya aandike ujumbe kuhusu perfume hiyo, huku akimsifia Diamond kwa kufanya vitu vikubwa pamoja na kukiri kuwa yeye sio shabiki wake isipokuwa anaupenda muziki wake.

“Sikuwahi kuwa mshabiki wa msanii huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema hapo nyuma kidogo, japokuwa nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia nimegundua kuwa, this young man is not only a good entertainer, but also a talented entrepreneur and businessman".

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.