Header Ads

Breaking News
recent

Viwanja vya ndege 10 vilivyo bora zaidi duniani kwa mwaka 2017.

10: Frankfurt Airport – Ujerumani
Miongoni mwa airport zilizokuwa busy Ulaya Frankfurt Airport ipo na inakamata nafasi ya 10 kwenye Skytrax World Airport Awards 2017.
9: London Heathrow Airport – Uingereza
London Heathrow Airport ndiyo airport iliyokuwa busy zaidi Ulaya kwa kusafirisha abiria wengi na katika Skytrax World Airport 2017 inakamata nafasi ya 9.
8: Zurich Airport – Switzerland
Katika list ya 2017 Zurich Airport imeanguka nafasi moja baada ya 2016 kukamata nafasi ya 7.
7: Chubu Centrair International Airport – Nagoya, Japan
Chubu Centrair International Airport upo umbali wa mile 22 kusini ya Nagoya katikati ya Japan na unakamata nafasi ya 7, kwa mujibu wa SkyTrax.
6: Hamad International Airport – Doha, Qatar
Ulifunguliwa rasmi 2014 na sasa Hamad International Airport iliyopo Doha imevuka nafasi nne na kukamata nafasi ya sita – mwaka 2015 ulikuwa katika nafasi ya 22.
5: Hong Kong International Airport
Uliwahi kushinda namba moja miaka ya nyuma lakini mwaka huu Hong Kong International Airport imeshika nafasi ya tano ikitetea nafasi hiyo iliyowahi kuikamata 2016.
4: Munich Airport – Ujerumani
Munich Airport imeanguka nafasi moja mwaka huu na kuifanya kuwa namba 4.
3: Incheon International Airport – Seoul, Korea Kusini
Incheon International Airport imekuwa katika tatu bora tangu 2013.
2: Tokyo International Airport Haneda – Japan
Haneda Airport inakamata nafasi ya pili ikiwa ni moja kati ya airport mbili kutoka Japan kwenye list hii.
1: Singapore Changi Airport – Singapore
Changi Airport umeshinda tuzo ya Skytrax World’s Best Airport kwa mara ya tano mfululizo ambapo miongoni mwa mambo yanayowavutia wasafiri ni uwepo wa ukumbi wa cinema ambao huonesha movie mpya kila siku bure, swimming pool na bustani nzuri ya vipepeo.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.