Header Ads

Breaking News
recent

UTAFITI: Mwitikio wa jamii pale ugonvi wa mwanamke na mwanamume unapotokea hadharani, unatofautiana.

Migogoro ya kifamilia bado ni tatizo kwa familia nyingi sana duniani kote, ambapo matokeo ya migogoro hiyo huweza kusababisha ndoa au mahusiano kuvunjika, magonjwa na hata kufikia vifo kutokea.

Ulevi, madawa ya kulevya, kukosa uaminifu, uchumi mbovu, kukosa ajira, kuchepuka, ubabe, ubinafisi, dhuruma, kiburi na manyanyaso mengineyo vimekua ni sehemu kubwa kwa familia na mahusiano mengi kuvunjika.

Pale inapotokea ugomvi wa wanandoa au wapenzi unawekwa hadharani, tena barabarani penye watu wengi, unafikiri nini kitakwenda kuwa ni matokeo hasa kwa shuhuda wa ugomvi huo?

Nimekutana hii video ya soflo iliyofanyiwa utafiti wakati ugomvi wa mwanamke na mwanaume unapotokea hadharani, je jamii inakuwa katika upande gani wa watu hawa wawili?

MATOKEO: Pale mwanaume alipoonekana kumpiga mkewe hadharani, kila mtu alijitokeza haraka na kuchukua hatua kwake ikiwa ni pamoja na kumpiga mwanaume huyo. Je nini matokeo kwa mwanamke alipompa kichapo mumewe hadharani?

MATOKEO: Pale ambapo mwanamke ameonekana akimpiga mumewe hadharani, hakuna hama mtu mmoja aliyejitokeza kumsaidia mwanaume yule asipigwe, zaidi ya watu kuchukua video na simu baadae wakapost mitandaoni!!

Watafiti hao wanasema kuwa, kila sekunde 37 zinazopita, mwanamume duniani huwa muhanga wa kudharirishwa na mwanamke.

Nivyema marafiki, wapenzi, wanandoa tukatafuta muafaka bila kudharirishana utu wetu mbele za watu wengi na ni vyema tukaepuka mambo haya ambayo huenda husababisha migogoro ya kifamilia yani ulevi, kukaa tu nyumbani bila shughuli, kuchepuka, ubabe, ubinafisi, kiburi na manyanyaso, dhurma, madawa ya kulevya, sigala na mengineyo.
 
 Sasa tupia macho video hii hapo chini ujionee mpango mzima.... 
 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.