Header Ads

Breaking News
recent

Siku ya wanawake duniani 2017

 Kila inapofika March 8 wanawake duniani kote husherehekea siku yao, huku dunia ikipata nafasi ya msingi kutathimini, mafanikio, mienendo, matokeo na stahiki wanazopaswa kupewa wanawake katika jamii.

Bado katika baadhi ya mataifa, mwanamke  bado hana haki ya hata kutoka kwenda kazini, sasa leo nimekutana na hii ripoti ya Shirika la Shirika la leba la kimataifa ILO likitujuza kuhusiana na utafiti kuhusu wanawake kutoka na kwenda kazini.....


Shirika la leba la kimataifa ILO leo huko Geneva limetoa ripoti, ikionesha kuwa watu wengi zaidi wanaunga mkono wanawake kufanya kazi nje ya nyumba.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na ILO kwa kushirikana na kampuni ya Gullup inaonyesha kuwa, asilimia 70 ya wanawake na asilimia 66 ya wanaume kati ya wahojiwa laki 1.5 katika nchi na sehemu 142 duniani, wanaunga mkono wanawake kufanya kazi zenye mapato nje ya nyumba.

Ripoti pia inaonyesha kuwa, wanawake na wanaume wenye kiwango cha juu cha elimu wanapenda zaidi wanawake kufanya kazi nje na kutunza familia kwa wakati moja.

Je vipi kuhusu Umoja wa Mataifa, wanaujumbe gani kuhusu siku hii ya wanawake duniani? Nimekuwekea video hii hapo chini kutoka Umoja wa Mataifa.....

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.