Header Ads

Breaking News
recent

Sehemu ya liliokuwa kaburi la Yesu kabla ya kufufuka, lafanyiwa ukarabati tena Israel.

Chumba kidogo kinachofunika kaburi ambako inaaminika Yesu Kristo alizikwa kimefunguliwa rasmi tena baada ya kufanyiwa ukarabati kwa miezi tisa.

Chumba hicho ambacho kinapatikana katika Kanisa la Kaburi la Yesu Kristo katika maeneo ya mji wa zamani wa Jerusalem kilikuwa kimekuwa dhaifu sana kiufundi.

Aidha, kilikuwa limebadilika rangi na kuwa karibu rangi nyeusi kutokana na masizi ya mishumaa mingi ambayo huwashwa eneo hilo.

Antonia Moropoulou, aliyesimamia ukarabati, amesema chumba hicho sasa kimepata tena rangi yake asili inayokaribia hudhurungi.

Chumba hicho kilifanyiwa ukarabati mara ya mwisho mwaka 1810.
Chanzo: BBC

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.