Header Ads

Breaking News
recent

Picha - Chris Brown avalia mavazi ya kiafrika.

 Mkali wa mindoko ya R&B na pop, Christopher Maurice maarufu kama Chris Brown kutoka Marekani ni kati ya wasanii wakubwa waliokwisha itembelea Afrika Mashariki katika shughuli zao za kimuziki.

Chris ambae mwaka uliopita alikwenda Kenya kupiga shoo, anaonekana katika picha hizi zilizotupiwa na mtandao mmoja hivi wa mitindo ya mavazi, akionekana kutupia mavazi ya kiafrika, huenda kwangu mimi ikawa mara ya kwanza kumuona akiwa katika mavazi ya kiafrika.
 Chris Brown ni msanii kutoka nchini Marekani, alizaliwa mwezi May 5 mwaka 1989 mjini Tappahannock, Virginia, Marekani, na kufikia mwaka 2002 alikua ameanza harakati za kutaka kutoka kimuziki.
Chris ni msanii wa kuimba, kurap, dancer, mwandishi wa mashairi ya muziki na mwigizaji pia. 

Lakini pia sio hivyo tuu, Chris ana mtoto mmoja na amekwisha jishindia tuzo kibao za muziki.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.