Header Ads

Breaking News
recent

Msanii Bow Wow kutoka Marekani atimiza miaka 30.

Msanii wa rap, muigizaji na mtangazaji wa runinga nchini Marekani Shad Gregory Moss, maarufu kama Lil Bow Wow au Bow Wow leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Bow Wow ni raia wa Marekani alizaliwa March 9, 1987, Columbus, Ohio, nchini Marekani na sasa anatimiza miaka (30)

Bow Wow alianza kufahamika kwa wapenzi wa muziki wa Rap toka mwaka 1993, akitengenezwa kimuziki na msanii mkongwe wa rap Snoop Dogg Dodgg.
Na kufikia mwaka 2000, Bow Wow aliachia album yake ya kwanza "Beware of Gog" ambayo ilifanya vizuri pia katika chati za muziki, wakati huo akiwa na umri wa miaka 13 tu na alisaini mchongo wa kurekodi akiwa na miaka 11.
 Baada ya hapo Bow Wow aliachia album nyingine ya pili mwaka 2001 iliyofahamika kama Doggy Bag.
 Kufikia mwaka 2003, Bow Wow aliachia album yake ya tatu Unleashed, ambayo ilikuwa ni album ya kwanza kuachia akiwa hatumii a.k.a ya Lil' katika jina lake. Baada ya hapo pia Bow Wow aliachia album kadhaa.

Bow Wow na Erica Mena Engagement
 Na pia kufikia Septemba 27, 2015, Bow Wow alijiunga na lebo ya muziki ya Bad Boy Records, aliyo hadi sasa, lebo hii inamilikiwa na msanii Puff Daddy.

Baadhi ya lebo alizo wahi kufanya nazo kazi ni pamoja na So So Def, Columbia, Cash Money, Republic.

Bow Wow pia amekwisha cheza movie na Tv series, movie yake ya kwanza ilikuwa inaitwa All About the Benjamins, in 2002, mwaka huo huo pia aliche za Like Mike, na mwaka 2004 alicheza Johnson Family Vacation na Roll Bounce mwaka 2005.

Bow Wow pia alicheza kama muigizaji msaidizi katika movie ya The Fast and the Furious: Tokyo Drift mwaka 2006 huku akionekana pia katika episodes tano za Entourage iliyokuwa ikirushwa kwenye Tv. 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.