Header Ads

Breaking News
recent

Movie za Seriese za Kikorea zazidi kuteka hisia za wapenzi wa filamu za nje.

Movie ni sehemu ya kiburudisho pale unapokuwa umepumzika, na watu wengi hupenda kuangalia movie pale wanapokuwa huru na wametulia nyumbani au hata sehemu za starehe, yaani baada ya kazi hupumzika na kuangalia movie wazipendazo na marafiki.

Hizi ni baadhi ya picha zinazotoka katika Seriese ya "BloodBath Island", ni filamu flani ya wadada watano walioigiza wanajeshi kutoka Korea ambao walikuwa wakipambana na maadui wao wakorea ambao nao upande wa pili walikuwepo wadada watatu hatari.
Katika tasnia hii ya movie wapo pia watu wanaojiita madj wa kutafsiri movie ambao tunaona wapo hapa nchini na hata Afrika Mashariki yote.
Wimbi hili la madj wa kutafsiri movie, limetoa mchango mkubwa sana katika kupromote kazi za nje hata kuliko za ndani.
Filamu za kitanzania kwa kiwango kikubwa huwa zinaigizwa kiswahili, sio mbaya ni sehemu pia ya kukuza lugha yetu, japo bado tunahitaji kuzisukuma kimataifa zaidi angalau basi kwa kuzitafsiri kwa lugha ya kiingereza, kama tunavyoona za nje zikipewa ukarimu hapa nchini.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.