Header Ads

Breaking News
recent

Huenda Eddy Murphy kuja na muendelezo wa movie ya Coming to America 2.

Coming to America ni filamu ya zamani ninayoweza kuitazama kila siku na isinichoshe kutokana na kisa chake cha kusisimua. Na sasa mashabiki wa filamu hiyo, tumepata habari njema.

Muigizaji wa filamu hiyo, Eddie Murphy ameonesha dalili ya kuja na muendelezo wake.

 Vyanzo vilivyo karibu na Eddie vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa muigizaji huyo yupo kwenye hatua za kwanza kuiandika.

 Bado haifamiki kama waigizaji wa mwanzo watarudi kwenye muendelezo wa filamu hiyo.

Muigizaji huyo alionjesha ujio huo kwa kuweka picha ya Vanessa Bell Calloway na kuandika: Coming to America sequel?” 

Tweet hiyo imeshafutwa pamoja na akaunti yenyewe kwasababu Eddie alikuwa amepanga kusema kitu kama hicho lakini si mapema hivi.
Source: Bongo 5

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.