Header Ads

Breaking News
recent

Floyd Mayweather kuzichapa ulingoni na Conor McGregor Las Vegas.

Mwanamasumbwi maarufu duniani kutoka nchini Marekani maarufu kama Mayweather anarejea tena ulingoni rasmi ikiwa ni baada ya kutangaza kuwa amestaafu mchezo wa masumbwi, sasa atazichapa na McGregor.

Floyd Mayweather na Conor McGregor watapigana Juni 10 Las Vegas, mwaka huu.

Mmarekani anayefahamika kama Money na Muireland aitwaye Notorious wameuteua ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas kuwa shehemu ya pambano lao.

Kila mmoja ametaja bei yake ya kupanda ulingoni kuwa dola za Kimarekani Milioni 100.

Mayweather amesema kwamba rasmi amerejea ulingoni kwa ajili ya McGregor baada ya kustaafu akiwa amepigana mapambano 49 na kushinda yote rekodi sawa na ya gwiji, legendary Rocky Marciano na hilo litaitwa "Pambano la Karne".

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.