Header Ads

Breaking News
recent

Uraibu wa simu wazidi kuongezeka kwa watumiaji wa Simu.

Unaweza kukaa muda gani bila kuwa na simu yako, kabla ya kuanza kuhangaika?

Mfano uwe umeisahau pahali, imeisha chaji au labda umelazimishwa kuizima na kuiweka mbali?

Wanasaikolojia wamegundua kwamba jibu lake litakuwa dakika chache sana - hasa iwapo umri wako ni kati ya miaka 18 na 26.

Baada ya kufanya utafiti, waligundua kwamba watu ambao walipokonywa simu walikuwa na uwezekano wa juu wa kuonyesha tabia ya "mfadhaiko" wakilinganishwa na watu walioachwa kukaa na simu zao.

Washiriki, baada ya kupokonywa simu zao, walipopewa simu - hata kama hazikuwa zao - walionesha kuwa na kiwango cha chini kidogo cha mfadhaiko.

Watafiti wanasema siku hizi watu wameanza kutumia simu kama mbadala badala ya kutangamana na watu.

Utafiti huo ulifanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Eotvos Lorand nchini Hungary.

Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa kundi la vijana wa miaka 18 hadi 26, ambao tabia zao zilinakiliwa kupitia video na mapigo yao ya moyo kupimwa.

Walipokonywa simu walionyesha dalili za mfadhaiko.

Matokeo yake si ya kushangaza, kwani simu yako ikiishiwa na chaji au uipoteze kwa muda, mwenyewe unfahamu kwamba unaweza kutatizika si haba.

Source:BBC Swahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.